Casemiro: Malengo yangu Kombe la Dunia na Kuirudisha United Juu

Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Brazil Carlos Casemiro ameweka wazi kua malengo yake makubwa kwasasa ni kushinda kombe la dunia na Brazil na kuirudisha Man United kwenye ubora.

Casemiro akifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari amesema kwasasa malengo yake ambayo amebakiza kwenye mpira wa miguu ni kushinda taji la kombe la dunia na kuirudisha Manchester United kwenye ubora wake.CasemiroKiungo huyo wa kimataifa wa Brazil amekua akifanya vizuri ndani ya klabu hiyo tangu atue klabuni hapo akitokea klabu Real Madrid ambapo amefanikiwa kuonesha utofauti mkubwa ndani ya timu hiyo.

Bashiri na Meridianbet wenye ODDS KUBWA na BOMBA kuliko sehemu yeyote ile kupitia tovuti yao au Bonyeza link hii https://app.mrdn.co/bashiri01

Casemiro pia wakati akizungumza na wanahabari amesema anafurahishwa na maisha ya jiji la Manchester ambapo hapo mwanzo alielezwa ni magumu lakini kwasasa anavutiwa zaidi kuwepo kwenye jiji hilo na kuitumikia klabu hiyo.CasemiroCasemiro pia alizungumzia suala la uongozi ambapo aliweka wazi kua anapenda uongozi kwenye timu kuongoza wenzake na kwakua pia anapenda kua mfano kwa wenzake uwanjani na hata nje ya kiwanja.

Acha ujumbe