Cedric Kaze na Soka la Kisasa

Soka la kisasa sio soka la kucheza kwa namba . Yaani lile soka la walinzi kucheza kama walinzi , viungo kusimama eneo lao na washambuliaji kusimama kama washambuliaji kwa majukumu ya namba zao .

Soka la kisasa limezaa mifumo mingi kwakuwa linaegemea katika majukumu zaidi na sio namba . Mfano sikuhizi ni nadra kuwapa viungo wakabaji asili ya Roy Keane , Viera , Chuji kwa hapa Tanzania na washambuliaji asilia kama Nteze John , Mmachinga kwa hapa Tanzania au Patrick Mboma pale Cameroon .

Soka la sasa halikupi fullbacks bali zinakupa wingback. Yaani haliegemei katika kucheza kwa namba zaidi bali jinsi gani utatimiza majukumu yako uwanjani.

Ozil pale Arsenal hivi sasa anaonekana si lolote si chochote si kwamba kwakuwa ameisha kwa kile kipaji chake kilichotufanya watu wote tumjue , bali amegoma kuendana na mabadiliko ya kimfumo na kimbinu katika soka la kisasa ambalo Arteta ni muumini wake. Arteta ameua majukumu asilia ya namba 10 na kulipanua eneo la ushambuliaji na kiungo cha juu kwa kuweka viungo na washambuliaji ambao wanacheza kama CMS ambao wapo flat .

Kwanini Zlatico Yanga ilimshinda?

Zlatico bado ni aina ya waalimu ambao wanaamini katika namba (tactical aspects) kinyume na soka la sasa ambalo limejikita katika majukumu uwanjani kimfumo na kimbinu (tactical and technical roles) . Zlatico alianza kuisuka Yanga katika ulinzi kuja eneo la kiungo kwa minajili ya kila mchezaji eneo hilo kusimama majukumu yake ya awali ya kwanza, ukabaji. Yanga ikawa (imekuwa) ngumu kufungika lakini hainyumbuki kimchezo kwa kuleta soka la kasi na muunganiko mzuri kimbinu.

Alikubali kina Yassin na Shomari Kibwana kwenye wacheze kwa asilimia kubwa kama fullbacks huku eneo la kiungo likiwa compact kwa viungo wakabaji zaidi ya watatu na wings zikitembea 50/50 huku eneo la ushambuliaji likiwa mbali kidogo na marking line kwa kutegemea mbinu za wings na CMs pale juu kutengeneza eneo kubwa kwa washambuliaji wa kati hali ambayo kwa mifumo ya wenzake waliiona Yanga kuwa na spaces nyingi inaposhambulia kwa maana ya namba ndogo ya attackers lakini inakuwa ngumu katiika ulinzi kwakuwa inakuwa na si chini ya wachezaji saba kwenye marking zone.

Jana katika mitandao ya kijamii , na vyombo vya habari , Yanga SC wamefanya usajili wa ghafla ambao haukutegemea hususani kipindi ambacho dirisha la usajili limefungwa . Yanga wamemsajili kiungo mshambuliaji mkongwe ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, Saidi Ntibazonkiza. Huyu ni mkongwe haswa katika soka kwa zaidi ya miaka 14, akicheza soka la ushindani nchini Burundi na Ulaya katika vilabu mbalimbali.

Sote tumesikia Yanga SC itampokea kocha wake mkuu kesho October 14, 2020 Bwana Kaze muumini wa soka la kisasa ka kutumia majukumu zaidi uwanjani kuliko namba. Yaani soka ambalo unakuta winga anarudishwa namba mbili na namba mbili anapanda juu , au unakuta namba 6 yupo mbele akicheza kama forward, kwa ujumla timu nzima inakuwa imejikita katika mambo mawili ya msingi , kufahamu jinsi ya kutumika katika mfumo na mbinu za kushambulia au kujilinda .

Saidi licha ya ukongwe wake, huyu anaweza kwenda kuficha udhaifu wa Carlos katika kukaba. Mfano, Kaze akaamua kumuingiza Carlos huru eneo la kati kwa kuwa 10 ikacheza na lone striker pembei akacheza Saidi juu yao Sarpong . Hapa Said atakuwa na kazi mbili kwa wakati mmoja , kwanza kuhakikisha wingback za timu pinzani hazipandi hapo amesaidia offensive patterns pia kuweka pressure kama invisible attacker huku Carlos akiwa huru ama flat eneo la juu kufanya link up ya eneo la kiungo na ushambuliaji au kudaka rebounds kwa surprise attacks .

Kaze amesikika akisema ile Yanga ametumiwa mikanda yake kwa mechi za karibuni akasema kuna mambo machache yanakosekana na mtu au watu wa kuyatenda. Je ni Saidi? Fikiria zaidi. Anaweza kuwa yeye au yeye kashauri aje ili kuwabadirishia majukumu watu kiwanjani, kupata balance nzuri katika kushambulia na kujilinda.

Itaendelea…


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua. 

Cheza sasa 

Samurai Ken Online Casino

 

29 Komentara

    Soka la sasa linaendeshwa kibiashara

    Jibu

    soka la sasa ilimradi club imeingiza pesa ndo linaangaliwa zaidi

    Jibu

    Hujio wa kaze yanga afrika utaleta mabadiliko ma kubwa

    Jibu

    Soka imepamba moto

    Jibu

    Kaze ni kocha mzuri

    Jibu

    Kaze anafanya vizuri

    Jibu

    Ngoja tuone kazi ya kaze ataipandisha daraja young afrika

    Jibu

    Soka limepamba moto

    Jibu

    safi

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Safi Sana naona soka limepamba moto

    Jibu

    Karibu Tanzania Cedric Kaze

    Jibu

    Game ya kisasa

    Jibu

    Kaze jembe

    Jibu

    Soka la kisasa pasi na kutengenez nafas

    Jibu

    Akaze buti sasa uko

    Jibu

    Karibu sana tanzania

    Jibu

    Yanga mbele daimaaa

    Jibu

    Kaze anafanya vizuri

    Jibu

    Karibu tz

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Soka la kisasa yanga wanaendanalo sawa tu

    Jibu

    ujio wa kaze yanga afrika utaleta mabadiliko

    Jibu

    Welcome KAZE cedric DAR young AFRICAN 1936. Nyuma mwiko Daima mwiko💪💪💪

    Jibu

    Inapendeza labla mabadiliko yata kuwepo

    Jibu

    👏🏼

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.