Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas amejiunga na klabu ya nchini Italia Como inayoshiriki ligi ya Serie B baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Ufaransa AS Monaco.

Mchezaji huyo mwenye miaka 35 wa kimataifa kutoka Hispania, awali kulikawa na taarifa kuwa alikuwa anatimkia kwenye ligi ya MLS nchini Marekani, kabla ya kushawishiwa na mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Dennis Wise ambaye ndio mkurugenzi mwendeshaji wa klabu hiyo.

Cesc Fabregas, Cesc Fabregas Kucheza Serie B, Meridianbet

“Nimekuja hapa kucheza kwa uwezo wangu wote na kushinda michezo mingi iwezekanavyo. Hiki ndio kipaumbele changu, kama ningehisi sihitajiki, ningetundika daluga.

“Nataka kuipeleka Como mahali inapostahili kuwepo, kwenye Serie A. Nimeamua kuja kwa sababu nyingi, nilihitaji mradi ambao utanipa shauku, sikuvutiwa na pesa. Wise alikuwa ndie mtu aliyenishawishi sana na naona mipango bora ya muda mrefu mbele.

“Nadhani hii ni moja ya changamoto muhimu kwenye maisha ya kazi yangu.” Alisema Cesc Fabregas

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa