Chama cha Soka Uingereza Champa Matumaini Tuchel

Chama cha Soka Uingereza kimeonyesha kuendelea kuwa na imani na kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza Thomas Tuchel wakiomba apewe muda zaidi wa kuinoa timu hiyo,

Chama cha Soka Uingereza Champa Matumaini Tuchel

Baada ya Uingereza kuondolewa jana kwenye michuano mikubwa Duniani dhidi ya Mabingwa watetezi Argentina, kumekuwa na presha kubwa ambayo ya kutakiwa kutimuliwa kwa Tuchel baada ya kushindwa kuipeleka timu hiyo Fainali.

Timu hiyo ilianza kupata goli la uongozi kupitia kwa Anthony Gordon katika dakika ya 55, kabla ya Argentina kuja kusawazisha katika dakika ya 85 kupitia kwa Enzo Fernandez na kisha ikapata bao la ushindi katika dakika za lala salama kupitia kwa Lautaro Martinez.

Kocha huyo amekuwa akilaumiwa kwamba uamuzi wa kutumia mbinu ya kujilinda baada ya kupata bao la kuongoza, ulichangia kuigharimu timu yake na hivyo afurushwe lakini FA imeonyesha kuwa na imani naye.

Chama cha Soka Uingereza Champa Matumaini Tuchel

Inaripotiwa kwamba FA haina mpango wa kufanya uamuzi wa mihemko na kuvunja mkataba na Tuchel na badala yake imepanga kuendelea naye.

Mpaka sasa hakuna uamuzi wowote kuhusu timu ya Taifa ya Uingereza juu ya kocha huyo wa zamani wa PSG na Chelsea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.