Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba SC, Clatous Chama amesema kuwa malengo yao msimu huu ni kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo Kaizer Chiefs wasitarajie mteremko katika mchezo wa kwanza wa robo fainali.

Jumammosi, Simba SC wanatarajia kushuka uwanja wa FNB Afrika Kusini kuwakabili wabishi Kaizer Chiefs, ambao wametinga hatua ya robo fainali wakitokea Kundi C.

 

chama, Chama :Malengo Yetu Fainali ya Ligi ya Mabingwa., Meridianbet

Chama amesema pamoja na kufahamu kuwa mchezo hautakuwa mwepesi kwa kila timu, hawatakubali kupoteza mchezo huo.

“Tumekuja Afrika Kusini kutafuta matokeo ili kujiweka katika nafasi nzuri tutakaporudi nyumbani katika mchezo wa marudiano ambao ndio utatoa hatima ya nani aende nusu fainali.”

“Haikuwa jambo rahisi kumaliza nafasi ya kwanza mbele ya bingwa mtetezi, ambaye ni kinara katika orodha ya timu bora Afrika, tumekuja huku kupambana kila mchezaji kiu yake ni kuona tunacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Chama

Chama aliongeza kuwa ubora wa kikosi chao unatokana na malengo waliyojiwekea na umoja uliopo, ambacho kimekuwa na muendelezo mzuri wa matokeo kuanzia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

chama, Chama :Malengo Yetu Fainali ya Ligi ya Mabingwa., Meridianbet

CHEZA HAPA

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa