Clatous Chota Chama ni mchezaji wa kutokea nchini Zambia ambaye ameliteka Soko la dirisha dogo la usajili hapa Bongo.
Ameliteka Soko Kutokana na umahiri wake uwanjani kipindi akiwa anawatumikia Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club Wana Lunyasi Kwa misimu mitatu mfululizo na kwa mafanikio yadidi.
Baada ya kutumika nchini Tanzania akiwa na Simba Kwa mafanikio zaidi “Real Clatous Chama” aliuzwa nchini Morocco Klabu ya Berkane.
Kutokana na mazingira ya nchini Morocco, Chama alishindwa kudeliver na sio kwamba ni sababu ameisha kimpira au ameshuka kiwango hapana ni Kwa sababu “Atmosphere” halisi ya mji wa Berkane imemshinda.
Mchezaji kung’aaa Klabu Moja Kwa mafanikio na Kwenda Nyingine akashindwa ni jambo la kawaida. Sio Chama wa kwanza ila wengi wamekuwepo na bado watakuwepo.
Pamoja na kucheza mechi chache sana ndani ya Berkane ila uwezo wake hauwezi kuulizwa maswali maana miaka mitatu aliyokaa Tanzania ndiye Mchezaji aliyependwa na Kila mpenda soka Tanzania hadi Fredrick Mwakalebela Makamu Mwenyekiti akasema wamemsajili Chama, huku Dismas Ten akitengeneza Tangazo la Mwamba wa Lusaka kuvaaa Jezi ya Yanga.
Cha kujiuliza Chama ni Faida (Asset) au Liability (Mzigo) akirudi Ndani ya Simba? Bado Clatous ni Asset Muhimu Sanaa Kwa Simba Kwa misimu miwili au mitatu mbele wakati Simba ikiandaaa vijana wengine kina Pape Ousmane Sakho.
Kabla ya Simba kuonyesha nia ya kumrudisha nchini kutoka Morocco, Yanga ndio walianza Kusema kuwa Mwamba wa Lusaka anarudi Jangwani. Sio mara Moja au Mbili Msemaji wa Yanga Haji Manara alisema, huku Injinia Hersi Said akionyesha Nia ya Kumsajili kiungo huyo ndani ya Yanga.
Pamoja na hao wawili Kusema hayo, hata Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mbatha amewahi Kuzungumza kuhusu Clatous Chota kuwa ni mchezaji mzuri na wanatamani kuwa nayeye ila wanaheshimu Mkataba wake na Berkane.
Sasa kumeibuka mashabiki walioshindwa kusimama na hoja na Kuanza kumponda Clatous Chota kwamba ameisha na hana jipya!! Niseme kuwa wanakosea sana maana uwezo wake unafahamika .
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA