Watu nane wanaongusha timu tofauti zinazo shiriki ligi ya EFL  nchini Uingereza   wamepimwa na kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Korona, EFL ya thibitisha.

Lilifanyika zoezi la kupima wachezaji na wahudumu wengine 2,213 kutoka katika vilabu 24 vinavyo shiriki kombe hilo, walioambukizwa  virusi vya Korona wanatoka timu sita zinazo shiriki.

Maelezo yaliyotolewa na EFL  yalisomeka kama ifuatavyo “Wachezaji na wahudumu wengine waliogundulika na maambukizi watatakiwa kujitenga kwaajili ya kupata matibabu kwa Muongozo utakao tolewa na EFL.

“Watakao ruhusiwa kuingia kwenye viwanja vya mazoezi ni wale ambao wamepimwa na kukutwa hawana maambukizi.

Championship ita rudi kuendelea siku ya jumamosi, siku tatu baada ya ligi kuu ya Uingereza kuanza, kwa hiyo watu wote walikutwa na maambukizi  watakosa kundi la kwanza la mechi.

Bentford ambao watawakabili Fulham wamethibitisha kuna mtu mmoja ambaye amekutwa na maambukizi lakini hawakuweka wazi kama ni mchezaji au laa.

Pia kunako ligi ya daraja la kwanza na la pili, wachezaji 428 na wahudumu walikutwa na maambukizi na kukamilisha idadi ya timu nane.

 

48 MAONI

  1. Habar ya kusikitisha sana kwa wapenz wa EPL kwan nimeingojea sana but cha msingi n kuomba MUNGU aepushe tatizo hili

  2. Habari mbaya ila tunatoa shukuru kwamba wamewekwa karantini wale ambao wanao corona na wengine kuruhusiwa kuendelea na mechi nijambo la kushukuru

  3. ila tutavuka nayo tu mechi zitachezwa case study ujerumani imefaulu na ligi imechezwa japo wapo waliopatikana na korona

  4. Hivi virusi vya covid 19 vimeharibu kila kitu hasa katika upande wa soka…ila tumuombe Mungu hakika tutasahau yote hayo

  5. Maoni:Hataree hii corona bado inaendelea kusumbua tunaomba mungu aliondoshe hili janga ili michezo iendelee maana michezo inasua sua kwaajili ya corona

  6. Ukisema uingereza kuna ligi nying hivyo bhasi kama championship itafungiwa isianze kucheza itabidi mapaka premier liga nayo kufungwa maana kuna timu zitapnda daraja kwenda primier ligi na wale walioshuka daraja primier ligi huenda championship,sasa kama champion itafungwa itahadhili kuikosaEPL

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa