Mshambuliaji wa Wigan Charlie Wyke mwenye umri wa miaka 29 alianguka wakati wa mazoezi ambapo moyo wake uliacha kupiga kwa dakika nne mwezi Novemba.

Charlie amewekewa kifaa cha kusaidia mapigo ya moyo “defibrillator” katika kifua chake kama Christian Eriksen ili kumruhusu kuendelea kucheza, ambapo alirejea wikendi iliyopita kwa kuanzia benchi.

Charlie Wyke: Eriksen Amenifanya Nirudi Uwanjani

Nyota huyo alisema kurejea uwanjani kwa Christian Eriksen kufuatia mshtuko wa moyo msimu uliopita kumemtia moyo wa kufuata nyayo zake.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Sky Sports (@skysports)

Katika hali ya kushangaza, kocha wa Wigan Leam Richardson alikuwa wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio kwa huduma ya kwanza hiyo imekuja baada ya wiki mbili ya wafanyakazi wa timu hiyo kupata mafunzo ya kujifunza jinsi ya kufanya matibabu ya kuokoa maisha.

Charlie Wyke: Eriksen Amenifanya Nirudi Uwanjani

Charlie aliiambia Sky Sports katika mahojiano maalum:”Ilikuwa siku ya kutisha zaidi maishani mwangu. Nilikuwa tu nikifanya mazoezi kama kawaida na kisha, ghafla, niliamka nikiwa sakafuni, mikono yangu imekatwa, nikiwa na wafanyakazi watano. Sikujua ni nini kilikuwa kimetokea.

“Kitu cha mwisho nilichokumbuka ni kwenda kwa kocha kumwambia nitaanguka lakini sikuweza kuyasikia maneno yangu. Kisha nikagundua baadaye kocha ndiye aliyeanzisha mchakato wahuduma ya kwanza na kunifanya nipumue tena”.

Charlie Wyke: Eriksen Amenifanya Nirudi Uwanjani

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alisema, anakumbuka akiwa likizo nikitazama yote yakitendeka dhidi ya Eriksen kwenye Euro na alikifikiria kuwa, ni lazima uwe na bahati mbaya kwa hilo kutokea kama mchezaji na kisha miezi minne baadaye ilimtokea mwenyewe.

“Lakini Eriksen amenipa msukumo wa kurejea. Kama asingerejea, sidhani kama ningekuwa na ujasiri nilionao. Ilinibidi kuona mtu mwingine akinifanyia hivyo ili niweze kujisukuma mwenyewe.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa