Charly Musonda Astaafu Soka Rasmi Akiwa na Miaka 28

Charly Musonda Jnr ametangaza rasmi kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 28, akiacha historia ya matumaini makubwa yaliyokatizwa na majeraha ya muda mrefu.

Charly Musonda Astaafu Soka Rasmi Akiwa na Miaka 28

Musonda kupitia mahojiano na Rising Ballers yaliyochapishwa Instagram, alithibitisha kuwa anaachana na soka. Alisema wazi kuwa amefikia mwisho wa safari yake uwanjani, safari ambayo ilijaa maumivu na mapambano yasiyoisha tangu alipoumia goti akiwa Uholanzi. Jeraha hilo lilikuwa kubwa kiasi cha kutishia kumaliza kabisa taaluma yake mapema, na sasa, imethibitika ndoto hiyo imefikia tamati.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Charly Musonda Astaafu Soka Rasmi Akiwa na Miaka 28

Musonda aliwahi kujiunga na Celtic kwa mkopo wa miezi 18 baada ya klabu hiyo kumpigia hesabu kwa muda mrefu. Alijitahidi kuingia kwenye mioyo ya mashabiki kwa kuvaa jezi namba 67 kama heshima kwa kikosi cha Lisbon Lions lakini aliishia kuonekana mara chache tu, ikiwemo mechi dhidi ya Hearts na pasi moja ya bao dhidi ya Zenit. Kocha Brendan Rodgers hakuwa na imani naye, hali iliyozidi kuzorotesha nafasi yake.

Baada ya kuondoka Celtic, maisha ya soka kwa Musonda yaliingia kwenye giza nene kwa kukumbwa na majeraha, kuachwa na vilabu, na kupotea kwa matumaini ya kuwa nyota mkubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.