Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich mali zake zote ambazo ziko ndani ya nchi ya Uingereza zimeshikiliwa na serikali ya nchi hiyo kutokana na kuwa karibu na rais wa Urusi huku klabu ya Chelsea ikiwemo kwenye mali zilizowekewa kikwazo.
Serikali ya uingereza inadai kuwa Roman Abramovich anahusika na siasa za Putin, aliiweka sokni klabu yake ili kuinusuru, lakini kutokana na vikwazo alivyowekewa hata weza kuiuza klabu hiyo bila ya kupata uthibitisho kutoka serikalini.

Klabu ya chelsea haitaweza kuuza mchezaji au kununua mchezaji yeyote wala kuwapatia mikataba mipya kwa wachezaji waliomaliza muda wao kwenye klabu hiyo, pia hawataweza kuuza tiketi zingine isipokuwa zile zilizouzwa kwa msimu mzima.
Pia Chelsea haitaruhusiwa kupata mapato ya hatimiliki ya matangazo ya Television inamaana klabu ya hiyo inaweza kupitia kipindi kigumu kwenye kulipa mishahara ya wachezaji na itabidi waanze kuwapigia mahesabu wachezaji makinda ambao wapo kwenye vilabu vingine kwa mkopo kama Armando Broja na Conor Gallagher.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.



