Ulikuwa usiku wenye presha na shamra shamra nyingi sana, ambapo vita ya matajiri wa Uingereza katika ardhi ya Ureno ila ni Chelsea ndio walioshinda kwa goli moja tu na kupeleka kombe London!

Historia imeandikwa tena na vijana wadogo kabisa walio chini ya Tuchel, kocha anayejulikana kubeba makombe na kuleta heshima katika kila klabu anayokwenda.

Katika mechi iliyohitaji shujaa, Kai Herverts anageuka shujaa huyo na kuisaidia timu yake kufanya poa na kubeba ndoo ya UEFA. N’golo Kante ameendelea kuthibitisha ubora wake kwa kuonesha thamani yake na kwanini ni kipenzi cha Tuchel baada ya kupata tuzo ya mchezaji bora wa mechi kwa kuonekana kila eneo la uwanja.

Chelsea wanafanikiwa kubeba ubingwa wa UEFA kwa mara ya pili sasa baada ya kufanya hivyo mwaka 2012 walipocheza dhidi ya Bayern Munich na ilikuwa penati ya Didier Drogba iliyoamua hatima vijana waliokuwa chini ya Dimateo kwa wakati huo.

Na sasa Chelsea wanabeba kombe huku wakionekana kutomiliki mpira sana lakini kila walipofika golini athari ilionekana, kwa kweli wamestahili ubingwa huu na watajivunia milele kufanya makubwa huku kila jina la shabiki wa timu hii litakumbuka makubwa ya mfaransa N’golo Kante!

BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa