Chelsea Haitasahau Maajabu Pale Munich Kwenye Fainali ya UEFA

Chelsea bila Terry, Ramires na Ivanovic ila kila mchezaji anaamini wanashinda mechi ile, Ndege inatua pale Munich Ujerumani, wanashuka na Mpiga picha wao Mathew Ashton na camera zake, Binadamu anaeenda kupiga picha matukio ya kutisha Allianz Arena

Usiku wa Mei 18, kuelekea fainali Kocha Roberto Di Mateo aliwaita wachezaji wote ukumbini, aliweka flash na video zikaanza kuchezwa, zilikua video za ndugu wa wachezaji wakiwapa hamasa, wengi walitokwa na machozi video ya Didier Drogba, walikusanywa vijana watatu kutoka Abdijan nyumbani Ivory Coast, Baba yao alibet shamba na nyumba hivyo Chelsea ikipigwa hawana pa kulala

Didier Drogba

Wakati taarifa zikiwa wazi David Luiz ni majeruhi, Garry Cahill ataanza na Ferreira muda wa warm up Luiz aliomba acheze, aliweka wazi licha ya maumivu ila anaomba awemo kwenye wanaume 11, Di Mateo alikubali ombi na Mtunza vifaa akaenda kuiandaa jezi ya Luiz, huku Betrand nae akianza usiku ule

Kabla ya kuingia uwanjani, Didier Drogba aliwaita wachezaji wote chumbani, alimuhitaji Lampard mbele, John Mikel, Ferreira na Peter Cech kisha akasema hii ni fainali yetu ya mwisho hii ni hatua ya mwisho, naombeni tupambane tuondoke kwa heshma kwenye mji huu

Wakati timu zinaingia uwanjani, Lampard na kitambaa chake mbele, uwanja ulijaa mashabiki wa Munich tupu, nyuma ya goli moja la Kusini walikuwepo Mashabiki wachache wa Chelsea, wakibeba mabango yao “John Terry with the Blue Army”, “Super Frank Lampard” “Drogba the African Elephant” wao walienda na imani kuwa ni fainali yao.

Dakika ya 83 ya mchezo baada ya machozi, jasho na damu Ni Thomas Mueller anaingia kambani, 1-0 kila mtu aliamini tayari mechi imeisha mashabiki wa Chelsea walikata tamaa, namtazam Roman Abramovich pale VIP kashika tama, Mwandishi Gabriel Clarke anafuta machozi

Lakini Mwanamama Teddy Fitcher hakukata tamaa anawaamsha mashabiki, Frank Lampard alimuita John Obi Mikel alimwambia “we cant loose here, we have to keep going”, nakumbuka Drogba alimtoa presha mtoto Bertrand alimwambia “Play the game not the ocassion” wakakubaliana wakaanzisha mpira

Ile corner ya Juan Mata, Drogba anapaa hewani na kuipeleka kambani, 1-1, ngoma inaelekea 120, Bavarians wanakuja na moto kwelikweli ila Chelsea bado wanapambana, dakika ya 95 Drogba anasababisha penalti, Cech anaicheza ile penalti, Abramovich alipagawa sana, aliona leo ni siku yake

Dakika 120 zilivyotamatika ilikua wasaa wa matuta, Di Mateo anaandaa list yake ya watu watano, ulikua wasaa wa maajabu ya Petr Cech na Didier Drogba, nazikumbuka hatua za Drogba kuelekea langoni

Mashabiki tumeshika tama, 1,2,3….Its Drogbaaaa! Namkumbuka Martin Tyler mtangazaji wa mechi hiyo alisema  “They have found the holy grail after adventure fought with danger, Drogba may never play for Chelsea again but will never be forgotten, Chelsea are the Champions of Europe” akimaanisha Chelsea wamepata walichokitafuta kwa jasho na Drogba anaweza asicheze tena akiwa na Chelsea ila jina lake halita sahahulika pale Stanford Bridge.

18 Komentara

    Drogba alikuwa ni mchezaji wa aina yake hakuwa mtu wa kukata tamaa

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    That night was the rise of African giant DIDIER DROGBA

    Jibu

    Chelsea wako vizuri Sana..

    Jibu

    Nakumbuka hii game mambo yalikuwa mooto meridian mmetisha mmenkumbusha mbal sana

    Jibu

    Ilikuwa bonge la game pale arenz arena b.munich anakufa kwake dk120 zinampa chelsea ushindi#meridianbettz

    Jibu

    Mpo vzr kwa taarifa

    Jibu

    Ilikuwa ni siku ya kusisimuwa na ya furaha sana kwa Chelsea.

    Jibu

    Didier goal drogba mmoja Kati ya shujaa katika game ile thanks meridian kwa update

    Jibu

    My goosebumps ….ilikuwa full game of inspiration ….nimeipenda sana hii meridiansport.co.tz

    Jibu

    chelsea naikubali sana chama langu

    Jibu

    Drogba “the African Elephant” huyu jamaa kaacha heshimsa kubwa sana kwenye soka la ulaya.

    Jibu

    Chelsea wako vizuri Sana..

    Jibu

    Mchezo mzuri sana

    Jibu

    Drogba the African elephat

    Jibu

    Chelsea wapo vizur sana

    Jibu

    Blues waliandika historia

    Jibu

    Drogba umeacha historia Sana ndani ya klabu ya Chelsea hongera Sana

    Jibu

Acha ujumbe