Chelsea Hatimae Wapata Ushindi

Klabu ya Chelsea baada ya kupitia msoto mkali hatimae wameweza kupata mattokeo ya ushindi mbele ya klabu ya Leeds United baada ya kuifunga klabu hiyo kwa bao moja kwa bila.

Chelsea sasa wanafanikiwa kupata ushindi wao wa pili katika michezo 16 iliyopita kwani klabu hiyo ilikua haijafanikiwa kupata matokeo ya ushndi kwa muda mrefu, Lakini leo kupitia goli la kichwa la beki wake wa katikati Wesley Fofana lilipeleka alama tatu muhimu darajani.ChelseaMatajiri hao wa jiji London licha ya kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wao dhidi Leeds United lakini pia walifanikiwa kuutawala mchezo huo, Huku wakitengeneza nafasi kadhaa za kufunga na kufufua matumaini upya ya klabu hiyo kuanza kuwania nafasi nne za juu.

Klabu ya Chelsea baada ya kushinda mchezo wa leo dhidi ya Leeds United wamefanikiwa kufikisha alama 34 huku wakiachwa alama 11 na klabu ya Tottenham ambayo inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Hivo wanahitajika kuhakikisha wanafanya kazi kubwa sana ili kuingia katika nafasi nne za juu.ChelseaKlabu ya Chelsea chini ya kocha Graham Potter wanatakiwa kuendeleza hichi walichokifanya katika michezo yao inayofuta ili kuwaweka katika nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao, Lakini wakiwa wanaendelea kuchechemea bado itakua changamoto kwa upande wao kushiriki michuano ya ulaya mwakani.

Acha ujumbe