Chelsea kuwauza Hudson-Odoi, Hakim Ziyech na Abraham

Chelsea wanatajwa kuwa wapo tayari kuwauza Callum Hudson-Odoi, Hakim Ziyech na Tammy Abraham wakati wa msimu huu wa uhamisho ili kufadhili uhamisho wa Erling Braut Haaland.

Blues inaendelea kuhusishwa na Haaland, ingawa inabakia kuonekana kuwa Borussia Dortmund wanada kuwa nyota huyo hataondoka kwenye soko la sasa.

Ikiwa dili litafanyika, inaweza kuwagharimu kikosi cha Thomas Tuchel angalau pauni milioni 150, na kwa mujibu wa Bild, mabingwa hawa wa Ulaya wanatarajia kukusanya takribani pauni milioni 90 kwa kuwauza Hudson-Odoi, Ziyech na Abraham.

Hudson-Odoi alipata wakati mgumu kuonesha mchango mkubwa huko Stamford Bridge kwenye kampeni ya 2020-21, akipata magoli matano tu katika mechi 37 za mashindano yote.

Wakati huo huo Ziyech, alifunga mabao sita na kusajili asisti nne katika mechi 39 za Blues kufuatia kuwasili kwake kutoka Ajax msimu uliopita wa joto.

Abraham, anayehusishwa na Aston Villa na West Ham United, alitikisa nyavu mara 12 msimu uliopita.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe