Frank Lampard huenda akarejea tena kwenye vichwa vya habari katika dirisha la usajili la mwezi Januari. Chelsea inasemakana kuongoza mbio za kuinasa saini ya David Alaba.

Alaba atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu baada ya maongezi ya mkataba mpya ndani ya Bayern Munich kugonga mwamba.

Beki huyu kisiki raia wa Austria, atakuwa huru kuzungumza na timu yeyote kuanzia Januari 1, 2021 na anaweza kusaini mkataba wa awali akitazamia kujiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea, Chelsea Inaongoza Mbio za Kumnasa Alaba., Meridianbet
David Alaba akishangilia kubeba taji la UEFA miongoni mwa mataji aliyobeba akiwa na kikosi cha Bayern Munich.

Chelsea licha ya kufanya makubwa kwenye dirisha la usajili lililopita, inatajwa ndio timu inayoongoza mbio za kuiwania saini ya Alaba wakichuana na Real Madrid,Juventus, PSG, Manchester City na Liverpool.

Kitu pekee kinachowapa nguvu The Blues ni uwepo wa wakala wa Alaba – Pini Zahavi ambaye anamahusiano mazuri na mmiliki wa miamba ya Stamford BridgeRoman Abramovic na wameshafanya biashara kwa miaka mingi.

Lampard anamtazama Alaba kama mtu sahihi atakayeongeza uzoefu kwenye safu yake ya ulinzi na huenda akamtumia zaidi kama beki wa kati wakati huu ambao Ben Chilwell anafanya vizuri kama beki wa kushoto.

Chelsea waliwasajili Hakim Ziyech, Timo Werner, Kai Havertz, Ben Chilwell, Edouard Mendy, Malang Sarr na Thiago Silva katika dirisha la usajili la majira ya joto.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Chelsea, Chelsea Inaongoza Mbio za Kumnasa Alaba., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa