Chelsea Kubeba Kiungo Leicester

Kocha mpya wa klabu ya Chelsea Enzo Maresca inaonekana anataka kufanya kazi na wanajeshi aliokua nao ndani ya klabu ya Leicester City msimu uliomalizika.

Klabu ya Chelsea inamfukuzia kiungo wa Leicester City Kiernan Drewsbury-Hall amefikia makubaliano na matajiri wa London kuhamia ndani ya klabu hiyo msimu wa mwaka 2024/25, Kiungo huyo amekubali kujiunga na klabu ya Chelsea na maslahi binafsi sio tatizo.ChelseaDrewsbury-Hall amekua na ubora sana ndani ya kikosi cha Leicester City ambapo amekua na mchango mzuri kuhakikisha klabu hiyo inarejea kwenye ligi kuu ya Uingereza, Jambo ambalo limefanya klabu ya Chelsea kutaka saini ya kiungo huyo.

Mchezaji huyo alikua anakaribia kujiunga na klabu ya Brighton and Hove Albion lakini dili hilo limevunjika kwakua kiungo huyo ameonesha wazi amevutiwa na kujiunga na klabu ya Chelsea, Hivo muda wowote matajiri hao wa jiji la London watamtangaza kiungo huyo.

Acha ujumbe