Mabingwa wa Ulaya, Chelsea wanatajwa kuwendelea kuwepo kwenye mbio za kuiwania saini ya nyota wa Borusia Dortmund Earling Haaland katika msimu huu wa joto

Bosi wa Chelsea, bwana Thomas Tuchel anasaka kuboresha safu yake ya mashambulizi na anataka kusajili kiungo mshambuliaji, hivyo Haaland anaripotiwa kuwa kipaumbele cha bosi huyu.

Vyanzo vya habari kutoka Chelsea vinaripoti kuwa klabu hiyo kwa sasa imewekeza nguvu kubwa katika kushughulikia dili la kinda huyu wa miaka 20 kutimba Stamford Bridge. Hata hivyo Chelsea wanatambua ugumu wa kukamilisha dili hilo msimu huu.

Chelsea Kukomaa na Earling Haaland

Taarifa zinasema kuwa klabu inaweza kujumuisha dili la kubadilishana mchezaji pamoja na pesa, litakalomuhusisha Tammy Abraham.

The Blues pia wamekuwa wakihusishwa na usajili wa nyota wa Spurs Harry Kane, pamoja na nyota wa Inter Milan, Romelu Lukaku.

Dortmund amefanya vyema katika msimu wake wa 2020-21 akifunga magoli 41 na kutoa usaidizi wa magoli 12 katika mechi 41 za michuano yote aliyocheza.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa