Chelsea Kutompiga Bei Jackson

Klabu ya Chelsea inaelezwa haina mpango wa kumuuza mshambuliaji raia wa kimataifa wa Ghana Nicklas Jackson kipindi hiki ambacho wanahitaji kupata mshammbuliaji mwingine.

Chelsea itaendela kubaki na Jackson kuelekea msimu ujao na inamuona kama sehemu ya mpango wao wa muda mrefu klabuni hapo, Taarifa zilikua zinaeleza kua mshamuliaji huyo alikua anaweza kuhusishwa kwenye dili la kumpata mshambuliaji mpya klabuni hapo jambo ambalo klabu hiyo imekanusha.chelseaMatajiri hao kutoka jijini London wako kwenye mpango wa kusajili mshambuliaji ambaye atakwenda kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho, Kwani uongozi wa klabu hiyo unaona bado washambuliaji waliopo klabuni hapo bado hawatoshi na ndio sababu ya kuingia sokoni kutafuta mshambuliaji mwingine.

Wakati Chelsea inaingia sokoni kutafuta mshambuliaji mpya imeamua kuweka wazi mapema kua mshambuliaji wake Jackson hatahusishwa kwenye dili lolote la kumpata mshambuliaji mpya klabuni hapo, Kwakua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana bado yupo kwenye mipango ya timu hiyo.

Acha ujumbe