Chelsea Kuuzwa Mwezi Huu.

Mwezi Machi umekuwa ni mwezi wa kihistoria kwa mashabiki wa Chelsea, Roman Abramovic anavuliwa umiliki wa klabu hiyo ndani ya siku chache zijazo.

Kabla ya tamko la kushikilia mali zote za Abramovic nchini Uingereza, bilionea huyo alishaweka wazi takwa lake la kuiuza Chelsea kwa kile alichodai kuwa, ni maamuzi magumu kwake lakini, yenye faida kubwa kwa klabu hiyo.

Fumba na kufungua, serikali ya Uingereza ikatangaza kuzifunga na kuzishikilia mali zote za bilionea huyo zilizopo nchini humo hii ikiwa ni sehemu ya kuonesha kutopendezwa na kinachoendelea nchini Ukraine.

Uingereza inaamini, Abramovic anamahusiano ya ukaribu zaidi na raisi wa Urusi na hivyo, katika kuonesha kuchukizwa kwao na vita inayoendelea Ukraine, Uingereza imeanza kuwashughulikia wafuasi wote wa Vladimir Putin waliopo nchini humo.

Kutokana na vikwazo alivyowekewa Roman Abramovic, hata uuzwaji wa The Blues ulisitishwa haraka na hivyo, klabu hiyo inafanya kazi kwa leseni maalumu ambayo haihusishi shughuli za kiuchumi klabuni hapo.

Lakini, maongezi yanayoendelea kati ya kampuni iliyokua imepewa jukumu la kusimamia uuzwaji wa timu hiyo na serikali ya UK, inaaminika kuwa, kuna uwezekano leseni ya sasa ikafanyiwa maboresho na hivyo, uuzwaji wa Chelsea unaweza kufanyika kuelekea mwishoni mwa mwezi huu.

Tayari kuna takribani ofa 20 zilizotolewa ili kuinunua klabu hiyo lakini, mchakato huu bado unaendelea katika ngazi ya serikali na kampuni ya ununuzi na usimamizi. Makubaliano ya pande hizi, yatatoa muelekeo wa mchakato huu.


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe