Chelsea Mawindoni kwa Nico Williamns

Klabu ya Chelsea imeingia mawindoni kumtafuta winga wa klabu ya Athletic Club ya nchini Hispania mwenye asili ya Ghana Nico Williams ambaye anafanya vizuri klabuni hapo kwasasa.

Winga huyo inaelezwa alikua kwenye mipango ya klabu ya Chelsea tangu dirisha kubwa lililopita kabla ya mchezaji Cole Palmer, Mpaka sasa mchezaji huyo amebaki kwenye orodha ya juu kabisa ya klabu hiyo licha ya kukosekana dirisha kubwa lililopita.chelseaDau la kupatikana kwa klabu hiyo ni kiasi cha Euro milioni 50 ambapo kama klabu yeyote itafika dau hilo itaweza kupata huduma ya mchezaji huyo, Hivo ni wazi klabu hiyo kutoka jijini London itarejea kuulizia huduma ya mchezaji huyo kwenye dirisha kubwa.

Mchezaji Nico Williams mwenye umri wa miaka 21 kwasasa amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Athletic Club, Huku akiwa moja ya wachezaji wa kutumainiwa zaidi ndani ya timu hiyo jambo lililofanya vilabu kadhaa barani ulaya kutamani kupata huduma yake.chelseaTaarifa zinaeleza klabu ya Chelsea haitakua yenyewe katika vita ya kumuwania Nico Williams kwani kuna vilabu kadhaa kutoka nchini Uingereza vinahitaji saini ya mchezaji huyo, Lakini bila kusahau mchezaji anawindwa na mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Hispania klabu ya Barcelona.

Acha ujumbe