Chelsea wameripotiwa kuwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski kabla ya uhamisho wa msimu huu wa joto.

Blues tayari wameanza kusaka fowadi mpya kabla ya kuanza kwa msimu ujao na mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland ndiye mmoja wapo katika malengo yao ya msingi.

Kwa mujibu wa Sky Sport News na vyanzo vingine huko Ujerumani, Chelsea walitaka kujua juu ya upatikanaji wa Lewandowski na wanatumaini wanaweza kumshawishi kuhamia Ligi ya Premia pale Stamford Bridge.

Chelsea Tayari Mazungumzoni na Lewandowski

Hata hivyo, mchezaji huyo wa miaka 32 anaripotiwa kuwa anapendelea kuhamia Uhispania ikiwa ataondoka Bundesliga msimu huu wa joto, lakini pia anafurahi kusalia Ujerumani na kuichezea Bayern.

Ikiwa Blues watashindwa kukubaliana kumsajili Lewandowski, basi wanaweza kutazama mipango mingine ikiwa ni pamoja na Erling Braut Haaland wa Borussia Dortmund, Harry Kane wa Tottenham Hotspur na Romelu Lukaku wa Inter Milan.

Lewandowski amekuwa na msimu mwingine mzuri mbele ya lango, akifunga mara 47 katika mechi 39 tu kwenye mashindano yote ya kampeni hii.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Lewandowski, Chelsea Tayari Mazungumzoni na Lewandowski, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa