Washindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Chelsea wameripotiwa kujiunga na mbio za kumsajili beki wa pembeni wa Inter Milan Achraf Hakimi.
Mabingwa wa Serie A wanaaminika kuwa wanataka kuuza karibu wachezaji wenye thamani ya pauni milioni 80 msimu huu wa majira ya joto ili kusawazisha vitabu vyao vya fedha, ikiwa ni sababu kubwa ya kuondoka kwa Antonio Conte mwezi uliopita.
Inter inamthamini mlinzi huyo wa Morocco kwa karibu pauni milioni 70 na kulingana na Daily Mail, Chelsea imekuwa klabu ambayo hivi karibuni kuungana pamoja na wapinzani wa London Arsenal na miamba ya Ligue 1 Paris Saint-Germain, kumfukuzia staa wao.

Meneja mpya aliyeteuliwa Simone Inzaghi anatamani Hakimi kusalia na miamba ya Italia msimu ujao, lakini klabu inaweza kupokea kwa kusita ikiwa ofa kubwa itawasilishwa msimu huu wa joto.
Hakimi alikuwa na kampeni ya kuvutia ya kwanza kwa Inter kama alivyokuwa muhimu kwenye kikosi cha Conte ambacho kilisaidia Nerazzurri kushinda taji lao la kwanza katika miaka tisa.
Mchezaji huyo wa miaka 22, aliyejiunga kutoka Real Madrid msimu uliopita wa kiangazi kwa karibu pauni milioni 40, alicheza mechi 37 kwenye Serie A, akifunga mabao saba na kutoa asisti 10 kama winga ya kushoto.
MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.