Chelsea Wahamia kwa Nico Williams

Klabu ya Chelsea baada ya kujitoa kwenye mbio za kunasa saini ya winga wa klabu ya Cystal Palace Michael Olise sasa wamehamia kwa winga wa klabu ya Athletic Club Nico Williams raia wa kimataifa wa Hispania.

Chelsea walikua wanamuhitaji winga Michael Olise lakini baada wakajitoa kwenye mbio hizo na winga huyo akaamua kujiunga na klabu ya Fc Bayern Munich ya nchini Ujerumani, Inaonekana nguvu zimehamia kwa kijana mdogo Nico W illiams mwenye umri wa miaka (21).chelseaWinga Nico Williams amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Athletic Club jambo ambalo limefanya vilabu kadhaa kumtolea macho barani ulaya, Mbali na Chelsea lakini pia klabu ya Barcelona wanaelezwa kumuhitaji sana winga huyo mwenye kipaji kikubwa.

Chelsea wanahitaji kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao chini ya kocha Enzo Maresca ili kufanya vizuri na kuepuka msimu mbaya ambao wameupata msimu uliomalizika, Hivo jambo kubwa ambalo wanalifanya kwasasa ni kuhakikisha wanaingia sokoni kutafuta wachezaji wenye ubora.chelseaMatajiri hao wa jiji la London wanaelezwa kua walikua wanamuhitaji Nico Williams tangu msimu uliomalizika lakini hawakufanikiwa kupata saini yake, Hivo msimu huu wanahitaji kuharakisha dili hilo kwakua wanajua fika wakichelewa wanaweza kumkosa mchezaji huyo kwakua wanaomuhitaji sio wao tu.

Acha ujumbe