Chelsea wanaripotiwa kuwa wameambiwa wanaweza kumsajili nyota wa Inter Romelu Lukaku ikiwa tu wataweza kufikia dau linalotajwa na klabu hiyo.

Nyota huyu raia wa Belgium amekuwa na msimu mzuri sana akiwa Inter, amefunga magoli 28 kwa msimu huu klabuni hapo akikamilisha idadi hiyo kwenye mechi dhidi ya Roma waloyopata ushindi wa 3-1 Jumatano.

Idadi ya magoli inahusisha magoli 22 ya Serie A, akiwasaidia Inter kupata taji lao la kwanza baada ya miaka 11.

Romelu Lukaku

Inter wanajikuta wapo kwenye hali ngumu kiuchumi, hivyo klabu inaweza kulazimika kuachana na wachezaji mmoja au wawili wakubwa kikosini hapo ili kuweka sawa hali yao ya kiuchumi, wakati baadhi yao wakiombwa kukubali kupunguzwa mshahara.

Kwa mujibu wa Corriere dello Sport, Lukaku ni miungoni mwa wale ambao wanatarajiwa kuathirika na hali hii na anaweza kuondoka ikiwa tu wanaomuhitaji watalipa dau la €120m.

Chelsea wametajwa kuwa wanaisaka saini ya nyota wao huyu wa zamani, ambaye amewahi kucheza mechi 15 akiwa pale Stamford Bridge. Manchester City pia wanahusishwa na uhamisho huo licha ya Pe Guardiola kusisitiza kuwa hawatafanya uhamisho wa pesa nyingi.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Lukaku, Chelsea Walipe 103 Kumpata Lukaku!, Meridianbet

CHEZA HAPA

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa