Imebainika kua klabu ya Chelsea walitoa ofa ndogo kwa klabu ya soka ya Ajax kwa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana Mohammed Kudus na ndio sababu iliyopelekea dili la mchezaji huyo kufeli.
Wakala wa mchezaji Mohammed Kudus ameweka wazi kua klabu ya Chelsea walihitaji huduma ya mchezaji huyo katika dirisha kubwa lililopita, Lakini ofa yao ndogo ndio iliyosababisha dili hili kutokamilika.Wakala huyo anabainisha walifanya mazungumzo na klabu hiyo katika kipindi cha usajili na walikubaliana mchezaji huyo akacheze Chelsea, Lakini kilichotokea ni kua matajiri hao kutoka jiji la London walitoa kiwango kidogo cha pesa kwa klabu ya Ajax ambacho hakikukidhi.
Klabu ya Westham United wao walienda na ofa nzuri kwa klabu ya Ajax ambayo ilikidhi vigezo vya klabu hiyo ambayo ilikua inammiliki mchezai huyo na hatimae wagonga nyundo hao wa London wakafanikiwa kupata saini ya mchezaji huyo.Wakala wa Kudus amesema ofa waliyoitoa Chelsea kwa Ajax ni kama walikua wanatania, Huku akieleza kua ukweli ni kwamba klabu hiyo ilimezwa au kutumia kiwango kikubwa cha pesa kwa Moises Caicedo na kushindwa kua na kiwango cha pesa kinachokidhi kwa Kudus.