Chelsea Wamfukuzia Kudus

Klabu ya Chelsea ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Ajax Amsterdam kwajili ya kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ghana Mohammed Kudus.

Klabu ya Chelsea bado haijaweka ofa kwa mshambuliaji huyo lakini inafanya mazungumzo na Ajax ili kuangalia uwezekano wa kumpata kiungo huyo ili boresha safu yake ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao.chelseaMohammed Kudus amekua kwenye kwango kikubwa sana ndani ya klabu ya Ajax baada ya kupata nafasi ya kuitumikia timu hiyo na kumfanya kuzivutia klabu mbalimbali barani ulaya kuhitaji saini yake.

 

Chelsea wanapambana kuhakikisha wanarudi kwenye ubora wao katika msimu wa 2023/24 na ndio sababu wanataka kusajili wachezaji wenye ubora mkubwa kuelekea msimu ili kurudisha makali yao.chelseaMohammed Kudus anawindwa pia na klabu ya Arsenal kutoka jiji la London hivo Chelsea wanapaswa kuhakikisha wanapeleka ofa mapema kwajili ya mchezaji huyo kabla majirani zao hawajawapiku kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana.

Acha ujumbe