Chelsea Wamvizia Camara, Monaco Yatoa Neno

Chelsea wanaendelea kufuatilia kwa karibu uwezekano wa kumsajili kiungo wa Monaco, Lamine Camara, huku Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Thiago Scuro, akikiri kuwa bado kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kuondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Camara alianza kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Marseille, licha ya Chelsea kuwa kwenye mazungumzo makali kuhusu uhamisho wake. Kocha Filipe Luis pia ameeleza wazi kuwa angependa kumbakiza kiungo huyo, lakini anakiri kuwa lolote linaweza kutokea kabla ya muda wa mwisho.

Chelsea Wamvizia Camara, Monaco Yatoa Ishara Kuhusu Mustakabali Wake

Hatma ya Camara huenda ikaunganishwa na kinachoendelea kwa Enzo Fernandez. Chelsea wanamwona Msenegal huyo kama chaguo la kuongeza nguvu kwenye kiungo, lakini uhamisho wake unaweza kutegemea iwapo Fernandez ataondoka Stamford Bridge.

Chelsea si klabu pekee inayomtaka Camara. Crystal Palace waliwahi kutoa ofa ya karibu £30m, huku Liverpool, Brighton na Nottingham Forest pia wakihusishwa na kiungo huyo mwenye umri mdogo.

Chelsea Wamvizia Camara, Monaco Yatoa Ishara Kuhusu Mustakabali Wake

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Monaco nao wako kwenye presha ya kufanya mauzo ili kuhakikisha wanatimiza masharti ya kanuni za kifedha. Kauli ya Scuro imeacha mlango wazi, huku muda ukiwa mchache sana kabla ya dirisha kufungwa.

Chelsea Wamvizia Camara, Monaco Yatoa Ishara Kuhusu Mustakabali Wake

Mbali na Camara, Folarin Balogun naye anaweza kuondoka Monaco. Everton wanamfuatilia mshambuliaji huyo, huku Arsenal ikiwa na kipengele cha kupata asilimia 17.5 ya ada ya mauzo endapo Balogun ataondoka Monaco.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.