Klabu ya Chelsea wanafikiria kumnunua golikipa mwingine huku taarifa zikisema kuwa watamchunguza Jordan Pickford kwenye Kombe la Dunia huku wakiendelea na kumchunguza mpaka mwisho wa michuano hiyo.

Kipa huyo wa Everton ameichezea Uingereza vyema katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 na Euro 2020, akicheza nafasi muhimu kwa kikosi cha Gareth Southgate. Pia amekuwa kwenye mazungumzo juu ya mkataba wake mpya huko Goodison Park, lakini bado hajaweka saini bado.chelseaMkataba wake wa sasa na Everton utaisha mnamo 2024 na wakati Toffees na Pickford wana nia ya kufikia makubaliano, ofa kutoka mahali pengine inaweza kumjaribu mchezaji huyo wa miaka 28 kuondoka klabuni hapo ikiwemo Chelsea.

The Sun inasema kuwa nia ya Chelsea ya kumtaka kipa huyo iko pale pale kwasababu mmiliki mpya wa klabu hiyo Toddy Boehly bado hajaridhishwa na kiwango cha Kepa Arrizabalaga na Edouard Mendy.

Kocha wa The Blues Graham Potter amempendelea Kepa kuliko Mendy, lakini The Blues pia wanamtaka kipa wake wa zamani wa Brighton Robert Sanchez kwaajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho laki ni je watacheza wote?chelseaMhispania huyo alijiimarisha kama mmoja wa walinzi bora chipukizi wa ligi chini ya Potter na yuko kwenye rada za Chelsea, lakini wanafahamu inaweza kuchukua ada kubwa kumzawadia kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 mbali na Pwani ya Kusini ndiyo sababu ya kutafuta njia mbadala.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa