Mustakabali wa mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo upo mbioni kumalizika huku akiwa na hatihati ya kuondoka klabuni hapo mwezi Januari, huku ripoti mbalimbali zikisema kuwa anaweza kutimkia Chelsea.
Ronaldo siku chache kadhaa alifanya kitendo ambacho kiliikera timnu yake baada ya kutoka nje ya uwanja kabla ya mchezo kumalizika kwenye ushindi wa 2-0 walipokuwa wakivaana na Spurs kwasababu hakucheza mechi.
Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amesikitishwa na hali yake msimu huu baada ya kujaribu kulazimisha kuondoka katika msimu huu kwasababu alitaka kushiriki Ligi ya Mabingwa lakini baada ya dirisha kufungwa aliamua kusalia klabuni hapo.
Ripoti mbalimbali ikiwemo Sunday World zinasema kuwa Cristiano anatazamiwa na kuhamia darajani kwenye dirisha dogo Januari. Mchezaji huyo wa Ureno ambaye mpaka sasa ana Ballon d’Or 5 akiwa nyuma ya Lionel Messi.
Kocha wa zamani wa Chelsea, Thomas Tuchel hakuwa na nia ya kufuatilia nia ya mmiliki wa Blues Todd Boehly kumtaka Ronaldo katika dirisha lililopita la usajili lakini baada ya Mjerumani huyo kuondoka, Chelsea wako tayari kufanya usajili huo huku wakivutiwa na rufaa kubwa ya kibiashara ya Mreno huyo.
Ripoti hiyo inadai kuwa Chelsea wameweka mkataba wa muda mfupi hadi mwisho wa msimu kwa Ronaldo, na chaguo la mwaka zaidi. Na Ronaldo yuko tayari kukubali kukatwa mshahara ili kufanikisha dili hilo pia.