Klabu ya Chelsea wametangaza jezi mpya ya mechi za nyumbani kwa msimu wa 2021/22.
Ikiwa ndiyo ‘taimu’ ambayo timu hutoa kezi zao za msimu mpya, na kuzivaa kwa maonesho mwishoni mwa msimu, Chelsea wameanza na uzi wao. Jezi hii inatarajiwa kutumika kwa mara ya kwanza kwenye fainali ya kombe la FA Jumamosi.
Tangazo rasmi la jezi hii mpya kutoka Chelsea, katika mfumo wa video limebeba ujumbe wa kingereza unaosomeka #ItsAChelseaThing.
Tangazo limewahusisha wachezaji wanawake na wanaume wa klabu, wakiwemo Mason Mount, Hakim Ziyech, Timo Werner, Pernille Harder, Sam Kerr na Fran Kirby.
Uzi huu mpya unatajwa kuwa umehamasishwa na urithi wa miaka ya sitini, umeandaliwa na Nike kwa ushirikiano na kampuni zinazoifadhili klabu. Bado soksi na bukta hazijaoneshwa, na zinatarajiwa kuwa na rangi za kawaida za blue na njano.
Jezi hii imepokelewa kwa maoni tofauti, baadhi ya mashabiki wameanzisha kampeni mitandaoni wakidai kuwa wanahitaji kurejeshwa kwa Adidas, na si Nike.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Uzi mkali
Jenzi nzuri sana
Jezi saf sana
Jenzi nzuri pia na bei iwe pouwa
Jezi nzuri Sana
Jezi kalii
Uzi umetulia
Uzi wa kibabe