Chelsea Yamsajili Lukaku Rasmi Kutoka Inter Milan.

 

Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa mshambuliaji hatari Romelu Lukaku kwa dau la pauni Milioni 97.5 (€115m) kutoka Inter Milan. Amesaini mkataba wa miaka mitano na atalipwa mshahara wa €12m pamoja na bonasi kwa mwaka.

 

Romelu amesema:” Nina furaha, nimebarikiwa kurudi kwenye klabu hii bora. Nimekuwa nikishabikia Chelsea nikiwa mtoto. Njia ambayo klabu inaenda inafaa matamanio yangu kikamilifu. Fursa hii inakuja kwa wakati unaofaa na tunaweza kupata mafanikio mengi pamoja ”.

Baada ya kuachana na Chelsea mnamo 2014, Lukaku alikua mmoja wa washambuliaji mahiri zaidi barani Ulaya, akifunga mabao 87 katika michezo 166 ya Everton kati ya 2014 na 2017, na mabao 42 katika mechi 96 wakati wa miaka yake miwili akiwa Manchester United kabla ya kusaini Inter mnamo 2019.

Mchezaji huyo wa miaka 28 alifunga mabao 24 kwenye Serie A msimu uliopita, akiisaidia Inter kutwaa Scudetto yao ya kwanza katika miaka 11 wakati klabu ikiimaliza utawala wa miaka tisa wa Juventus kama mabingwa wa Italia.


SHINDA NA TIKI REWARD KASINO

Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!

Tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe