Chelsea The Blues wamefikia maamuzi ya kumtimua aliekua kocha wao Thomas Tuchel mapema siku ya leo.

Hali hii imekuja baada ya timu hiyo na mfululizo wa matokeo mabovu tangu kuanza kwa msimu huu kitu ambacho kimewafanya mabosi wa timu hiyo kufikiria kumuondoa kocha huyo.

chelseaNdimu ilikamuliwa kwenye kidonda zaidi siku ya jana kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya ambapo Chelsea ilipoteza kwa goli moja kwa bila dhidi ya Dinamo Zagreb ya nchini Croatia.

Mabosi wa klabu hiyo wamefanya usajili wa gharama majira haya ya joto ili kuijenga timu hiyo lakini msimu ulipoanza mambo yamekua sio mazuri kabisa ka upande wao mpaka sasa wameshapoteza michezo mitatu miwili ndani ya ligi kuu ya uingereza na mmoja kwenye ligi ya mabingwa ulaya.

Tuchel anaondoka Chelsea akifanikiwa kuipa timu hiyo mataji kama Ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2021, taji la Uefa super cup, pamoja na lile la klabu bingwa ya dunia pamoja na kucheza fainali mbili za na fainali moja Carabao cup.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa