Klabu ya Chelsea imepata majanga tena baada ya taarifa ya beki wake wa kushoto na nahodha msaidizi wa klabu hiyo Ben Chilwell raia wa kimataifa wa Uingereza kupata majeraha.
Ben Chilwell amepata majeraha ya nyama za paja ambayo yanakadiriwa kumueka nje ya uwanja kwa muda wa takribani miezi miwili, Hivo klabu ya Chelsea itamkosa mshambuliaji wake huyo.Klabu hiyo kutoka jiji la London imekua kwenye wakati mbaya sana tangu msimu uliomalizika, Wakiwa wameuanza msimu huu vibaya huku majeraha yakiendelea kuwaandama ndani ya kikosi chao.
Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua akisumbuliwa na majeraha tangu atue klabuni hapo akitokea klabu ya Leicester City, Licha ya kuonesha kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo kila anapopata nafasi.Chelsea itakua na wakati mgumu katika miezi miwili ambayo Ben Chilwell atakosekana kwenye kikosi hicho, Lakini inaelezwa jopo la makocha ndani ya klabu hiyo wanafurahishwa na kiwango anachokionesha beki mbadala wa klabu hiyo Marc Cucurella.