Chelsea Yapata Plan B Ya Haaland Kutoka Euro 2020

Timu ya Chelsea imepata mchezaji atakayekuwa kama mbadala au plab B ya kocha Tuchel endapo watshindwa kukamilisha usajili wa nyota wa Borussia Dortmund, Erling Haaland.

Dili la Chelsea kumdaka mchezaji wa Borussia Dortmund Haaland limekuwa halieweki kutokana na timu hiyo kuonekana kutokuwa tayari kumuachia mchezaji huyo kwa bei ya chini.

Kocha Tuchel amepata mbadala endapo dili kumpata Erling litapotea au endapo halitofanikiwa, Chelsea watakuwa mbioni kufuata nyayo za muhispania Moreno anayekipiga katika timu ya villarreal.

Moreno yupo katika michuano ya Euro 2020 akiwa na Spain, huku akiwa hajafanikiwa kufunga goli hata moja licha ya kupata kucheza dakika 90 katika mechi ya pili ya michuano ambapo walitoka sare kwa goli la Morata.

Akiwa na Villarreal, Moreno alipachika mabao 23 kwenye Laliga msimu uliopita na kuisaidia timu yake kubeba kombe la Europa League baada ya kufunga katika fainali dhidi ya Man United.

Je, Moreno anaweza kuwa ni usajili sahihi kwa timu kubwa kama Chelsea ambayo ipo kwenye kipindi kizuri huku ikidaiwa kuwa straika wao, Tammy Abraham pia anaweza kutimka klabuni hapo?


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe