Chelsea Yatoa Kipigo kizito

Baada ya kupokea kichapo kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza leo klabu ya Chelsea imetoa adhabu kali kwa klabu ya Wolverhampton baada ya kuichabanga kwa mabao sita kwa mawili.

Mchezo wa leo ambao Wolves walikua nyumbani ulianza kwa Chelsea kutangulia kupata bao kupitia kwa Nicklas Jackson, Kabla Matheus Cunha kusawazisha matajiri hao wa London walipata bao la pili kupitia kwa Cole Palmer kabla ya Wolves kusawazisha dakika za mwisho kipindi cha kwanza kupitia kwa Jorgen Larsen na mchezo kwenda mapumziko kwa sare.chelseaKipindi cha kwanza ilionekana mzani kua sawa lakini kipindi cha pili ubao uligeuka kwani vijana wa Enzo Maresca walionekana kuchachamaa kwelikweli, Kwani dakika ya 49 tu Noni Madueke anaweka goli la tatu kabla ya kufanya hivo tena dakika ya 58, na 63 na kuwapa The Blues uongozi wa mabao matano kwa mawili.

Klabu hiyo iliendelea kutoa adhabu ambapo mchezaji Joao Felix ambaye alitokea benchi alifanikiwa kufunga goli la sita dakika ya 80 ya mchezo huo, Huku nyota Noni Madueke na Cole Palmer wakitakata kwenye mchezo huo Palmer akihusika na mabao manne akifunga moja na kutoa pasi tatu za mabao huku Madueke akifunga mabao matatu.chelseaKlabu ya Chelsea sasa wanakua na alama tatu baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Manchester City lakini leo wakionekana kuimarika kwenye eneo lao la ushambuliaji kwa kiasi kikubwa, Kazi kubwa ikifanywa na kocha Enzo Maresca kwani ndio ambaye amebadilisha kikosi hicho ndani ya muda mfupi na kuonekana hatari mbele ya lango haswa katika mchezo wa leo.

Acha ujumbe