Klabu ya Chelsea ipo mawindoni kwajili ya mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa raia wa kimataifa wa Colombia Jhon Duran ambaye amekua sio chaguo la kwanza ndani ya klabu ya Aston Villa.
Klabu ya Chelsea ipo mezani kwasasa ikifanya mazungumzo na klabu ya Aston Villa kwajili ya kumpata mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia, Matajiri hao wa London wanataka kuboresha safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao.
Mshambuliaji Jhon Duran amekua hapati nafasi mara kwa mara ndani ya Aston Villa hivo kupata nafasi ya kuondoka klabuni hapo na kupata nafasi ya kucheza itakua ni jambo la muhimu sana upande wake, Kinachosubiriwa kwasasa ni kama klabu hizo mbili zitaafikiana juu ya mshambuliaji huyo.