Klabu ya Chelsea tayari imeshakubalina makubaliano binafsi na mchezaji wa klabu ya Manchester City Raheem Sterling na inasemekana kuwa makubaliano hayo yanaenda kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye klabu hiyo.

Chelsea kazi waliyobaki nayo kwa ajiri ya kukamilisha usajiri huo ni Manchester City, ambapo sasa kazi imebaki kwenye mazungumzo tu ya ada ya uhamisho huo, huku kwenye mwaka mmoja aliobakisha anaweza kuondoka kwenye viunga vya Etihad kwa ada isiyopungua £45million.

Chelsea, Chelsea Wanaweza Kumfanya Sterling Kuwa Mchezaji Anayelipwa Zaidi Darajani?, Meridianbet

Mpaka sasa kwenye viunga vya Stamford Bridge, mchezaji aliyebakia ambaye analipwa zaidi ni Ng’olo Kante ambaye anapokea takribani £290,000 kwa wiki, ambapo awali alikuwa ni Romelu Lukaku ambaye amepelekwa kwa mkopo nchini Italia kwenye klabu ya Inter Milan.

Endapo Sterling atafanikiwa kutua kwenye viunga vya Stamford Bridge, basi atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye klabu hiyo.

Klabu ya Chelsea inatarajia kufanikisha uhamisho huu mapema zaidi na kuweza kumjumuisha kwenye kikosi kitakachokwenda na timu hiyo kwenye michezo ya pre-season nchini marekani ambapo safari inatarajiwa kuanza siku ya Jumamosi.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa