Klabu ya Chelsea, Arsenal, na Tottenham Hotspurs wametolewa kwenye kombe la ligi maarufu kama Carabao usiku wa kuamkia leo. Ilikua ni siku mbaya vilabu vya London kutoka kwenye michuano hiyo.

Klabu ya Chelsea ambao walikua Ugenini wakicheza na klabu ya Manchester City huku wakiruhusu kufungwa mabao mawili kwa bila, Magoli ya Riyad Mahrez pamoja na Juliano Alvarez.chelseaKatika mchezo huo klabu ya Manchester City ilionekana kutawala mchezo huo huku vijana wa Graham Potter klabu ya Chelsea wakionekana kuzidiwa huku pia wakishindwa kuweka mipango ya kuweza kupata alama tatu muhimu na wakaambulia kipigo cha mabao mawili.

Klabu ya Arsenal nao waliambulia kipigo cha mabao matatu kwa moja wakiwa katika dimba lao la nyumbani, Mabao ya Danny Welbeck,Jeremy Sarmiento, pamoja na Tariq Lamptey yalitosha kuipa ushindi Brighton Hove Albion huku bao la kufutia machozi la klabu ya Arsenal likifungwa na Eddie Nketiah.chelseaVijana wa Antonio Conte nao walitupwa nje kwenye michuano ya Carabao Cup baada ya kufungwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Nottingham Forest. Mabao ya Renan Lodi na Jesse Lingard yaliiwezesha klabu ya Nottingham kufuzu hatua inayofuata kwenye michuano hiyo.

Jana haikua siku nzuri sana kwa vilabu kutokea jiji la London kwani vilabu kutoka jijini humo vimetupwa nje ya michuano hiyo.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa