Chido Obi Martin Akamilisha Vipimo vya Afya Man United

Aliyekua mshambuliaji wa timu ya vijana ya Arsenal mwenye kipaji kikubwa Chido Obi Martin (16) amefanikiwa kukamilisha vipimo vyake vya afya ndani ya Man united.

Chido Obi Martin amekua akionesha ubora mkubwa sana ndani ya timu ya vijana ya Arsenal licha ya kua na umri mdogo wa miaka 16 tu, Klabu ya Manchester United ilivutiwa na mchezaji huyo kinda na kumshawishi ajiunge na klabu yao wakimuahidi kumpatia nafasi ya kucheza kwenye timu ya wakubwa.

chido obi martin

Klabu ya Arsenal inaelezwa ilipambana kwa kiwango kikubwa kuhakikisha wanambakiza kinda huyo ndani ya klabu yao na kumpa ofa ya mkataba mzuri, Lakini walizidiwa kete na Man United ambao inaelezwa walimuahidi maslahi mazuri lakini pia mchezaji huyo kuona ni rahisi kupata nafasi ndani ya United kuliko Arsenal.

Miaka ya hivi karibuni wachezaji kutoka timu za vijana wamekua wakipata nafasi kwenye timu ya wakubwa kwa kiwango ndani ya Man United tofauti na Arsenal, Mwaka jana tu mchezaji Kobbie Mainoo alipata nafasi kwenye timu ya wakubwa na mpaka sasa ameingia kwenye kikosi cha kwanza hii inaelezwa ndio sababu kubwa iliyomvutia mchezjai huyo.

Baada ya kukamilisha vipimo vya afya kinda Chido Obi Martin atasaini mkataba sasa wa kuitumikia klabu ya Manchester Uited ambao bado haujajulikana ni wa miaka mingapi, Lakini kabla ya kusaini mkataba kuna hatua ambazo Man United wanapaswa kuzifuata kulingana na taratibu za ligi hiyo.

Acha ujumbe