Chini ya Miaka 20 Wenye Thamani Kubwa ya Uhamisho

Katika soka kila kipindi huwa na historia yake ambayo kwa namna fulani huwa imejengwa ndani ya wachezaji ambao ndio hubeba falsafa nzima ya soka. Katika siku za karibuni baadhi ya nyota wa mchezo wa soka wamekuwa wakiibuka na kuonesha uwezo wao wa hali ya juu sana na kuzifanya baadhi ya timu kupishana kuwafukuzia ili kuweza kupata huduma zao.

Huu unaweza kuwa mwaka mzuri wa raia wa taifa la Uingereza ambao kwa hakika wamekuwa na msimu mzuri sana na wenye mafanikio makubwa kwao. Wachezaji kama Jadon Sancho na Declan Rice ni kizazi ambacho taifa hilo linawahitaji na hakika waneweza kuwa na thamani ya aina yake katika soka hata pale watakapoa amua kuzihama klabu zao hizo watauzwa kwa thamani ya pekee sana.

Jadon Sancho, nyota huyu ambaye aliweza kuachana na Manchester City na kuamua kujiunga na Borussia amekuwa na msimu mzuri sana huku akiweza kuzama golini kwa kufunga mara 11 na kutoa pasi za magoli 17. Thamani yake imeweza kupanda hadi kufikia €150.3 milioni kwa klabu itakayomhitaji.

Matteo Guendouzi, akiwa amesajiliwa kutoka Lorient ambaye aliweza kusajiliwa na Arsene Wenger kutokana na uwezo wake wa kuchezesha timu jambo ambalo Wenger alishindwa kulifumbia macho kabisa. Kwa sasa thamani ya nyota huyo imeweza kupanda hadi kufikia  €70.1 milioni huku akiwa tayari amecheza mechi 44.

Nicolo Zaniolo, klabu ya AS Roma inajivunia kuwa na aina ya wachezaji wa aina hii ndani ya kikosi chao ambao kwa hakika umri wao bado unawaruhusu kufanya makubwa hata kwa baadaye. Kutokana na uwezo wake ameweza tayari kupanda thamani na kushika mioyo ya wana-Roma. Thamani yake imeweza kufikia €67.4 milioni.

Kai Havertz, nyota wa Bayer Leverkusen ambaye amekuwa na msimu wa pekee sana ndani ya kikosi chake hicho. Akiwa tayari amefunga magoli 15 na pasi za magoli nne katika mechi zake 32 alizocheza ndani ya Bundesliga. Hadi sasa thamani yake imeweza kupanda hadi €64.3 milioni. Kutokana na uwezo wake aliweza kuwavuta Munich kutenga dau la €100 milioni.

Declan Rice, awali kabisa aliweza uuteka moyo wa kocha wa taifa wa Uingereza Southgate kwa kumwomba ahame kuchezea timu ya taifa ya Ireland na ajiunge na upande wa timu yao. Umri wake na mambo anayoyafanya yanaonesha ana mwangaza wa kufanya makubwa sana hapo mbeleni. Thamani yake hadi sasa ni €64.2 milioni.

Nyota wengine walio chini ya umri huo wanaotazamiwa kufanya vizuri na wakiwa tayari na thamani kubwa hadi sasa ni Gianluigi Donnarumma thamani ya €59.4 milioni, Vinicius Jr. mwenye thamani ya €55 milioni, Justin Kluivert thamani ya €44.3 milioni, Evan N’Dicka mwenye thamani ya €44.1milioni na Ryan Sessegnon mwenye thamani ya €43 milioni. Wote hawa wanahitaji dau kubwa sana ili kuweza kuwasajili wakiwa bado katika umri wa kawaida sana.

Acha ujumbe