Cristian Chivu alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutoa heshima zake kwa Franco Baresi kuelekea mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu kati ya Inter Milan na Manchester City, akimtaja gwiji huyo wa zamani wa Milan kama “mmoja wa watu wakubwa waliowahi kuwa alama” katika soka.

Kwa mujibu wa taarifa kupitia njia rasmi za Inter, kocha huyo alianza mkutano wake na waandishi wa habari mjini Hong Kong, ambako timu hizo zitakutana kwenye uwanja wa Kai Tak Stadium siku ya Jumamosi, kwa kutoa salamu za rambirambi kwa Baresi, aliyefariki siku ya Ijumaa akiwa na umri wa miaka 66.
“Tunaungana na ulimwengu wa michezo kutoa pole kwa familia ya Franco Baresi. Kila anayependa soka amepoteza mtu mkubwa aliyekuwa alama ya mchezo huu.” Alisema Chivu
Akihamia kwenye masuala ya uwanjani, Chivu alisema ilikuwa “furaha kubwa sana” kujiandaa kwa msimu mpya katika mazingira hayo, licha ya timu zote mbili kuwa bado hazijafikia kiwango chao kamili cha utimamu wa mwili baada ya kufanya maandalizi kupitia kambi ya mazoezi nchini Ujerumani.
Kocha huyo alionyesha furaha kubwa kuhusu usajili wake mpya, John Stones, ambaye amejiunga na mabingwa hao kama mchezaji huru.
“Nina furaha na kuwasili kwa Stones. Ni mchezaji muhimu kwetu kwa sababu nyingi: ubora wake, haiba yake na uwezo wake wa kuongoza,” alisema Chivu. “Anaongeza kiwango cha safu yetu ya ulinzi.
Huku dirisha la usajili likiwa bado limebakiza takribani mwezi mmoja kufungwa na baadhi ya wachezaji wakiwa bado hawajarudi kutoka kwenye mapumziko baada ya Kombe la Dunia, Chivu ameweka wazi kuwa kikosi chake bado kinaendelea kujengwa na hakijakamilika.

Tunahitaji uvumilivu. Ninaomba kiwango kiendelee kupanda,” alisema Chivu, akiongeza kuwa Inter itaendelea “kutathmini fursa zilizopo” za kuongeza wachezaji wengine wenye uwezo wa kuifikisha timu hiyo katika hatua nyingine ya juu zaidi.
Mwisho, Chivu alitoa maneno ya heshima kwa wapinzani wao wa Jumamosi na kocha wao mpya, Enzo Maresca, ambaye amechukua nafasi ya Pep Guardiola katika kikosi cha Manchester City.
“Tayari ameshinda Championship na Kombe la Dunia la Vilabu. Ni kocha kijana, lakini tayari amefanya vizuri sana,” alisema Chivu. “Ninaamini yeye ndiye mtu sahihi wa kuiongoza klabu hiyo baada ya Guardiola.”

