Chris Wilder Kutemana na Sheffield United.

Imeripotiwa kuwa kocha mkuu wa Sheffield United, Chris Wilder anatarajia kuachana na timu hiyo.

Hii ni baada ya timu hiyo kufanya vibaya msimu huu licha ya kumaliza nafasi ya 9 kwenye msimamo wa EPL msimu uliopita.

Wilder ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Sheffield United, alipatiwa kibarua cha kukinoa kikosi hicho mwaka 2016 na alifanikiwa kuipandisha timu hiyo kwenye EPL msimu uliopita.

Kiwango cha Sheffield msimu huu kimekuwa ni duni maradufu wakati huu ikiwa ni timu inayoshika mkia ikiwa na pointi 13 pungufu ya timu iliyopo kwenye nafasi ya kusalia kwenye EPL msimu ujao.

Wilder baada ya kuipandisha Sheffield United kwenye Ligi Kuu Uingrereza, EPL.

Pamoja na sababu mbalimbali, iliwahi kuripotiwa kuwepo na hali ya sintofahamu kati ya Chris Wilder na mmiliki wa timu hiyo, Prince Abdullah kwa kile kilichodaiwa kuwa, Prince Abdullah anaamini amewekeza kwenye timu kwa kusajili wachezaji kama Ryan Brewster na Ollie McBurnie lakini hakuna walichokifanya msimu huu.

Mtazamo wa Prince Abdullah unapingwa na Wilder ambaye amekuwa akisema hajapatiwa kile alichokihitaji katika kuitengeneza timu hiyo msimu huu. Hii imejidhihirisha kwenye madirisha mawili ya usajili msimu huu ambapo timu hiyo haijasajili wachezaji wenye uwezo wa kuinusuru msimu huu.

Wilder anakwenda kuachana na timu yake ya utotoni baada ya kuiongoza kwa miaka 5, nani atakayechukua mikoba ya kocha huyu pengine na kuinusuru Sheffield United wakati huu ambao zimebaki mechi 10 tu msimu huu kukamilika?


Ni Burudani Iliyokithiri na Mkwanja Nje Nje Katika Mchezo Halisi wa Chicago Gold.

Fanikisha malengo yako bila kuumiza kichwa, tengeneza mkwanja bila wasiwasi na kasino ya Meridianbet. Jiunge sasa Ufurahie Chicago Gold kasino.

CHEZA HAPA

10 Komentara

    Duuh

    Jibu

    Mhhh

    Jibu

    Naona kaamua

    Jibu

    Hapo kazi ipo

    Jibu

    Maisha mema

    Jibu

    Bora aachane nao mana wamemzingua sana

    Jibu

    Atali sana

    Jibu

    Majanga

    Jibu

    Duu mbona hatari

    Jibu

    Duuh sio poa

    Jibu

Acha ujumbe