Chris Wood Sikuweza Kuikataa Newcastle

Chris Wood amekubali kuwa haikuwa rahisi kukataa uhamisho wa kwenda Newcastle baada ya kuulizwa kuhusu kuhamia kwenye klabu hiyo ambayo iko kwenye hatari ya kushuka daraja.

Kulikuwa na sintofahamu kwenye klabu ya Lancashire pale tu kulipozuka taarifa ya  Magpies kuwa wamefanikisha usajiri wa mchezaji wa kimataifa wa New Zealand, ambaye kwenye mkataba wake kuna kipangere cha kuvunja mkataba chenye thamani £25million huku uhamisho wa ukiwaacha Burnley na hali mbaya.

Chris Wood
 Chris Wood

Chris Wood alisisitiza kuwa alikuwa hana budi kukubali nafasi ya kucheza kwenye klabu hiyo, hamasa ya mmiliki mpya na matumaini ya mwanzo mpya ndivyo vilivyomfanya ahamie kwenye klabu ya Newcastle, alipoulizwa kwenye mkutano wa waamdishi wa habari kuhusu kuondoka klabu ya Burnley jioni ya alhamisi alijibu.

“Haukuwa uhamuzi rahisi, nafikili ni nafasi adhimu, nilitumia miaka minne na nusu pale nilikuwa na furaha sana nikiwa pale, wachezaji wenzangu wafanyakazi na klabu yote kwa ujumla ilikuwa bora sana kwangu.

“Kiukweli, nilikuwa natarajia kuwa ningeachwa pale tu Burley ilipopanda ligi, lakini hivyo ndivyo inavyokuwa na ndivyo mpira ulivyo muda mwingine, hakuna anayeweza kupanga vitu hivi, unapaswa kuangalia tu nini kiko mbele yako na unafanya nini na mpira kwa muda fulani.” Alisema Chris Wood


 

JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe