Beki wa Chelsea, Andreas Christensen alijitoa kucheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Liverpool licha ya beki huyo kutokuwa na majeruhi, beki huyo hakuhusika kwenye kikosi cha mechi iliyofungwa Jumamosi kwa mikwaju ya penalti 6-5.

Thiago Silva alicheza akiwa na maumivu ya tatizo la goti alilolipata wakati wa pambano la Wembley, huku Malang Sarr na Cesar Azpilicueta kwenye safu ya ulinzi ya The Blues wakiwa kwenye benchi.

 

Christensen, Christensen Aligomea Kucheza Fainali ya FA., Meridianbet

Christensen yuko tayari kukamilisha uhamisho wa bure kwenda Barcelona msimu utakapokamilika, baada ya kudumu kwa miaka kumi huko Stamford Bridge.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekabiliana na matatizo kadhaa ya majeraha na ugonjwa katika wiki za hivi karibuni, lakini kujiondoa kwake kwenye mchezo Jumamosi kumeacha picha mbaya kwa Blues.

Chelsea watawakaribisha Leicester siku ya Alhamisi na Watford Jumapili katika harakati za kumaliza katika nafasi ya tatu ya Ligi ya Premia, huku uwepo wa Christensen haujulikani.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa