Matajiri wa klabu ya Manchester City ambao ndio wamiliki wa kampuni ya City Group wapo kwenye mazungumzo na wana hisa wanaomiliki klabu ya Palermo ya nchini Italia kwa ajiri ya kuinunua klabu hiyo.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa mazunguzo kuhusu mauziano ya klabu hiyo kati ya City Group na Palermo yameanza siku ya Jumatano ya tarehe 15 june 2022, na mpaka sasa makubaliano ya msingi tayari wameshafikiana.

City Group

Klabu ya Palermo mwaka 2019 walifirisika na kushushwa mpaka kwenye ligi ya semi-professional Serie D. Wiki iliyopita walifanikiwa kushinda mchezo wa play-off ambapo sasa wamefanikiwa kutoka Serie C na kuingia ligiya  Serie B kwenye msimu utakaoza mwezi August.

City Group na msimazi wa klabu ya Palermo Dario Mirri, walikubaliana kuwekezeza kiasi cha €13milion, pia pesa hiyo inaweza kuongezeka kulingana na mahitaji ya klabu, huku tayari wameshaa mchakato wa kuajiri wafanyakazi wapya ambao wataanza michakato ya kusuka mbinu mpya za kuisaidia klabu hiyo kupanda ligi kuu ya Serie A.

City Group wameanza mipango kwa ajiri ya klabu ya Palermo, tayari wameanza kufikilia kumpa kazi aliyekuwa kocha wa timu ya vijana Leandro Rinaudo, kuwa mkurugenzi wa michezo pamoja Giorgio Zamuner, wakati Giovanni Gardini atachukua nafasi ya Rinaldo Sagramola kama mkurugenzi wa mtendaji.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa