City: Guardiola Ana Karata 1 Tu Ndani ya Miaka Mitatu

Mnamo tarehe 14 Februari, 2020, ilikuwa ni siku mbaya zaidi kwa wapenzi na mashabiki wa Manchester City inayoongozwa na Pep Guardiola. Siku iliyoitwa ya Wapendanao kwao ilikuwa ni zaidi ya kutafuna mizizi michungu kabisa tena isiyotibu chochote kwa City.

Siku mbaya kwa Man City

Kwani siku hiyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) lilitangaza kuwazuia Man City kutokukushiriki mashindano hayo kwa miaka miwili mfululizo, 2020/2021 na 2021/2022. Man City walivunja kanuni ya matumizi mabaya ya pesa (financial fair play) au FFA kwani walitumia pesa nyingi zaidi kuliko wanachoingiza katika kipindi cha 2012 hadi 2016. Licha ya kutumia pesa nyingi ila Man City waliandaa takwimu ya kuonesha kiasi kilicho sahihi yaani kichache zaidi ili mradi kuipiga chenga kanuni ya FFA.

UEFA walifanya uchunguzi mwaka 2019 na kubaini kosa hilo hivyo kuwapa adhabu hiyo pamoja na faini ya dola milioni 30 ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 60 za Kitanzania. Ijapokuwa mwanya wa kukata rufaa upo wazi kwa Man City kudhihirisha kwamba wao wapo sahihi, maisha bwana hela zako mwenyewe na zinakutesa!

Sheria zinahusikaje hapo kwa Guardiola?

Kimsingi wenzetu wanajali sana sheria zao kwani FFA ipo kwa lengo la kuweka usawa baina ya timu ndogo na kubwa katika usajili, pia kuhakikisha timu zinajiendesha kwa faida ili kuepuka kufirisika.

Si unajua ule usemi wa hela ya deni usiipige hesabu za kimatumizi, ndiyo haswaa, si ya kujitegemea maana waweza kulipwa au mdaiwa akaingia mitini. Hivyo City itabidi wafunge mkanda na wapigane kindakindaki kuhakikisha wanatwaa kombe hilo UEFA Champions League msimu huu huku wakisikilizia rufaa yao. Mashabiki wanachotaka ni furaha na furaha hiyo inaweza ikazima machungu ya kufungiwa kuliko kutoka kapa kabisa.

Hapa itabidi Guardiola aamue tu kuwa punda afe mzigo wa bwana ufike yaani kwa hali na mali City watwae taji hilo kwa mara ya kwanza msimu huu.

Mechi ya Man City na Real Madrid

Utamu wa muwa ni kifundo, haswaaa, ndivyo tunavyoweza sema kwani licha ya Man City kukabiliwa na shtaka hilo pia inawalazimu kupambana na Real Madrid katika hatua ya 16 bora. Hapa hatuzungumzii tu Madrid na City bali makocha wao ndiyo vita kubwa zaidi. Zidane na Guardiola ni mahasimu haswa tangia enzi wakiwa wachezaji huko Uhispania, mmoja Madrid na mwingine Barcelona.

Uzuri ni kuwa wote wanafundisha soka kulingana na falsafa ya klabu zao nguli huko Uhispania. Guardiola yeye anafundisha (Tiki Taka Style) yaani soka la pasi nyingi, kucheza kitimu, kukaba na kushambulia kwa kasi. Huku Zidane akitumia mbinu ya kushambulia kwa kushtukiza zaidi akitegemea mawinga.

Vikosi na majeruhi kuelekea UEFA

Ama kweli kufa kufaana, kwani Guardiola ananufaika na majeraha ya winga Gareth Bale na Eden Hazard hivyo kumpa kibarua kigumu Zidane kuwatumia Isco, Asensio, Vinicius Jr na Mariano ambao wote si wazoefu.

Ila kwa upande wa City yeye ana wachezaji wake wote hatari kama B. Silva, Aguero na Gabriel Jesus. Kwa upande wa kiungo nyasi zitawaka kwa Modric, Kroos na Casemiro watakabiliana na Fernandinho, D. Silva na Mahrez wa City na hakika patachimbika kweli kweli.

Hivi unaanzaje kukosa kwa mfano?

Mechi ni tamu sana

Ingawaje kuna utofauti mkubwa baina ya Madrid ambao wamechukua kombe hilo mara 13 tofauti na City ambao hajapata hata moja ila mpira si historia . Historia zimeweka ili zivunjwe, ndiyo tunavyosema mtaani.

Uzuri wa soka ni kama baiskeli ukishajua umejua ila ubaya wanasema mpira unadunda. Je, Guardiola atatumia karata yake vizuri dhidi ya Madrid au ndiyo tutegemee huruma ya UEFA katika rufaa?

Ingia uwanjani leo ukiwa hapa hapa kwetu uone!

29 Komentara

    City washinde Ndio vizuri

    Jibu

    Asante meridianbet #kwa taarifa

    Jibu

    Maoni:asanteni sana #meridianbettz kwa taarifa.

    Jibu

    Hizo mechi zilikuwa mechi ya kuingiza mkwanja mrefuuu

    Jibu

    Asante meridian kwa makala

    Jibu

    Mechi za hela#meridianbettz

    Jibu

    Guadiola ni kocha ambae ana kikosi bora

    Jibu

    Msimu wa pesa ushaaza

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Hizi mechi zilitupa hela watu wengi

    Jibu

    hela#meridianbettz

    Jibu

    Asante kwa habari

    Jibu

    Sheria ni muhimu kufatwaa

    Jibu

    Duuh makala nzuri

    Jibu

    Muda wa kusaka pesa

    Jibu

    Nice update 👍# meridianbet

    Jibu

    Ukiwa na meridianbet pesa nje nje

    Jibu

    Hizi ni figisu figisu sababu Gadiola alisema league ya uingereza ni nyepesi mno.

    Jibu

    Pole yao kwetu kawaida tu

    Jibu

    Sijawahi ipenda City #Meridianbettz

    Jibu

    Maoni:duh it’s so sad Kwa cc mashabik wa city

    Jibu

    Sheria ifatwe

    Jibu

    👏

    Jibu

    Makala nzuri

    Jibu

    Ikiwa itathibitika pasi na shaka kwamba walivunja kanuni za FFA hata washinde UCL msimu lungu la UEFA haliwaachi salama

    Jibu

    duh kwer mtihan Kwa gadiola

    Jibu

    Vizur

    Jibu

    Hahahahaha huyo kocha nae alizid kebeh sana huwez kwenda nchi ya mtu kufanya kazi alafu unaleta maneno yako yasiyo eleweka ina maana yeye ni zaid ya wengine acha lungu la UEFA limpitie wamekua wakitumia pesa kwa ajili ya usajili si ya kutoka ndan ya club n nje ya miradi mingine

    Jibu

    Makala manzuri

    Jibu

Acha ujumbe