City Wainunua Lommel SK

Kampuni mama ya Manchester City imefikia makubaliano ya kununua timu ya Ligi Daraja la pili Ubeligiji Lommel SK.

Ni klabu ya tisa kuingia kwenye orodha ya vilabu vinavyomilikiwa na City Football Group (CFG), ambayo inamiliki hisa ya timu za United States, Japan, Australia na China.

Taarifa zinasema wiki iliyopita, CFG imekubali kulipa deni la klabu lenye thamani ya £1.75m kama sehemu ya makubaliano.

Wachezaji wa Lommel SK

Mmiliki wa Man City, Abu Dhabi United Group, ndio ana hisa nyingi kwenye CFG. Hisa zilizosalia zinamilikuwa na taasisi za Marekani na China.

Lommel walikuwa nafasi ya sita katika msimamo wakati msimu wa Ubeligiji ukimalizika kwasababu ya janga la Corona. Wanacheza katika uwanja unaoingiza watu 8,000 kaskazini mshariki ya Ubeligiji.

CFG ununuzi wake wa hivi karibu ulikuwa Indian Super League klabu ya Mumbai City FC Novemba mwaka jana.

“Ubeligiji ni moja nchi zinazosakata kabumbu bora Ulaya na imepelekea mafanikio makubwa kwenye timu ya taifa, na wametengeneza wachezaji bora duniani, wengine tunawafahamu vuzuri sana, kama  Kevin de Bruyne na Vincent Kompany,” amesema Mtendaji Mkuu wa CFG, Ferran Soriano.

“Uwekezaji huu ni sehemu ya mipango ya muda mrefu kuwa nchini inayosakata kabumbu kwa viawango vya dunia, kucheza soka la kuvutia na kuendeleza vipaji.

“Tumevutiwa na tamaduni, vifaa vya mafunzo na uwajibikaji kwenye soka la vijana na tunatazamia kujifunza kutoka kwenye mbinu zao na kusaidia klabu kupata mafanikio kwenye miaka ijayo.”

CFG inamiliki vilabu:

Manchester City
New York City
Melbourne City
Yokohama F Marinos
Montevideo City Torque
Girona
Sichuan Jiuniu
Mumbai City

3 Komentara

    Habari nzuri

    Jibu

    Ni habar njemA Sana kwa wapenzi na mashabiki wa city dunia Asante meridian kwa habar za kimichezo

    Jibu

    habari njema

    Jibu

Acha ujumbe