Manchester City wako kwenye kasi ya ajabu kuelekea kumsaini kiungo chipukizi Ayyoub Bouaddi kutoka Lille na sasa wamewapita Arsenal kwenye mbio za kumnyaka kinda huyo. Hii inaenda kuwa hadithi ya usajili yenye presha na ubabe wa mabingwa wa England wanaotaka kuunda kizazi kipya cha mastaa.

Kwa mujibu wa taarifa za Sky Sport, City wameongeza nguvu kwenye mazungumzo, wakikimbiza dili hili kwa kasi ya juu. Arsenal walikuwa mbele kwenye mbio hizi, lakini uamuzi wao wa kuhamia kwa Bruno Guimaraes umeacha njia wazi. City wakaingia, wakapiga hesabu zao, na sasa wako hatua moja tu kutoka kumchukua Bouaddi, kijana mwenye umri wa miaka 18 ambaye tayari amekubaliana masharti binafsi ya mkataba wake mpya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mazungumzo kati ya mkurugenzi wa michezo Hugo Viana na rais wa Lille, Olivier Letang, yamekuwa moto usiozimika. Simu zinapigwa mchana na usiku, ofa za maneno zinatupwa mezani, lakini Lille hawajalegea hata kidogo. Wanataka €100m kamili, bei ya mchezaji wa dhahabu. City wanajaribu kushusha hadi €90m pamoja na bonasi, na hapo ndipo kikwazo kikubwa cha kifedha kinapokaa kama ukuta wa mawe.

Bouaddi ana mkataba wa muda mrefu hadi 2029, lakini moyoni tayari ni mchezaji wa City. Ameikubali dili nono litakalomfanya abaki Etihad hadi 2031. Kijana huyu aling’aa kwenye Kombe la Dunia akicheza kwa Morocco, akivuta macho ya mashabiki na makocha kwa utulivu wake, ubunifu na uwezo wa kudhibiti mchezo kama kiungo aliyekomaa. Ingawa hajafunga bao lolote kwenye mechi zake 96 za Lille, City wanaona kitu kikubwa ndani yake.


