Kwa mujibu wa Daily Star, klabu ya Manchester City wana nia ya kumleta nyota wa Brighton Alexis Mac Allister Etihad.
Nyota huyo wa safu ya kati amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka kwa Seagulls tangu aliporejea kutoka Qatar akiwa na medali ya mabingwa wa Kombe la Dunia na Pep Guardiola anaweza kumleta dirisha la usajili litakapofunguliwa.
Mac Allister mwenye miaka 24, ameshiriki katika mechi 19 za Ligi kuu ya Uingereza kwa timu hiyo ya Pwani Kusini msimu huu, akifunga mara tano huku vijana wa Roberto De Zerbi wakiendelea kung’ara.
Brighton kwa sasa wanashikilia nafasi ya nane lakini wana nafasi ya kuwapita Liverpool na Fulham mbele yao watakapocheza mechi zao za mkononi.
Na mchezaji huyo wa Kimataifa wa Argentina amekuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya hali ya juu ambayo yameifanya klabu hiyo kupata ushindi wa kuvutia dhidi ya Chelsea, Liverpool na Manchester United mnamo 2022-23.
Guardiola anaamini kuwa kiungo huyo atakuwa kiungo bora kwenye kikosi chake cha hadhi ya Kimataifa na atakuwa tayari kufikia thamani ya Brighton ya pauni milioni 70.
Mhispania huyo anataka kukiboresha kikosi chake baada ya msimu wa wastani hadi sasa kuwaacha mabingwa hao wakiiwinda Arsenal kwa ajili ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Mkataba wa Mac Allister utaendelea hadi 2025, na kuifanya Seagulls kudhibiti hali hiyo mbele ya kile kinachotarajiwa kuwa msimu mwingine wa shughuli nyingi wa matumizi kwa vilabu vingi.