Claudio Ranieri Akalia Kuti Kavu Watford.

 

Klabu ya Watford imeanza mchakato wa kutafuta mrithi wa Claudio Ranieri anayetaka kutimuliwa kufuatia kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Norwich siku ya Ijumaa.

 

Vyanzo vya karibu vya klabu hiyo vinatarajia Ranieri atapoteza kibarua chake huku Hornets sasa wakitafuta mbadala wake.

Sportsmail ilifichua kuanzia mkesha wa mwaka mpya kwamba Muitaliano huyo alikuwa katika shinikizo kubwa pale Vicarage Road huku kukiwa na shaka juu ya nafasi yake kama kocha mkuu.

Watford sasa inaaminika kukaribia kumwachisha Ranieri kutokana na rekodi mbaya ya kushinda mara mbili pekee kati ya mechi 14 chini ya meneja huyo wa zamani wa Leicester na Chelsea.

Ranieri, 70, aliomba msamaha kwa mashabiki baada ya Norwich kufanya vibaya, amepoteza michezo 11 tangu achukue nafasi ya Xisco Munoz mnamo Oktoba.

Watford wamevuna alama moja pekee katika michezo nane iliyopita na kuporomoka mpaka nafasi ya 19 katika jedwali la ligi kuu wakiwa wamecheza michezo mitatu zaidi ya Burnley inayoshika mkia.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe